Jumatatu 25 Mei 2026 - 11:30
Muungano wa Mapinduzi ya Februari 14 wa Bahrain: Vita vya usafishaji Bahrain ni mwendelezo wa mauaji ya kimbari yanayofanyika Ghaza na Lebanon

Hawza/ Baraza la Kisiasa la Muungano wa Vijana wa Mapinduzi ya Februari 14 wa Bahrain limesisitiza kwamba; kile kinachoendelea kwa sasa nchini Bahrain ni vita vya usafishaji wa kikabila na kimadhehebu.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Baraza la Kisiasa la Muungano wa Vijana wa Mapinduzi ya Februari 14 wa Bahrain limesisitiza kwamba kile kinachoendelea hivi sasa nchini Bahrain ni vita vya usafishaji wa kikabila na kimadhehebu vinavyoongozwa na “mtawala dikteta Hamad” dhidi ya raia wa asili wa nchi hiyo, hususan wafuasi wa madhehebu ya Shia.

Baraza hilo lilisema katika taarifa yake kwamba; vita vya usafishaji vinavyoendelea Bahrain ni sehemu inayohusiana na vita vikubwa vya mauaji ya kimbari vinavyoshuhudiwa katika eneo hili; kuanzia Ghaza na Lebanon hadi vitisho vinavyofanana na hivyo ambavyo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inakabiliana navyo.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa; mradi wa mauaji ya kimbari unaosimamiwa na Wazayuni na Wamarekani una lengo la kufuta uwepo na utambulisho wa watu, kung’oa wakazi asili na kuweka badala yake mfumo wa utamaduni wa kujisalimisha na udhaifu, ili kufungua njia kwa ajili ya utawala wa madola ya kiburi na ya kikoloni.

Katika sehemu nyingine ya taarifa hiyo imeelezwa kwamba; Bahrain ni moja ya medani zinazowaka moto katika mpango huo wa uharibifu, kwa sababu wananchi wake daima wamekuwa mstari wa mbele miongoni mwa mataifa ya muqawama, na watoto wake bado wamesimama dhidi ya mradi wa wahalifu kama vile “Netanyahu na Trump”. Sauti yao na harakati yao ya kupinga uhalalishaji wa mahusiano, kufukuzwa kwa kambi za kijeshi za Marekani na kuangushwa kwa mtawala dikteta haitanyamazishwa.

Muungano huo, huku ukijivunia wananchi wa Bahrain ambao wamethibitisha uwepo wao katika kutetea wanazuoni na utambulisho wa taifa, ulisisitiza kwamba; kuendelea kung’ang’ania kufufua nembo za kidini na kuandaa majlisi na maombolezo ni uthibitisho kwamba mashinikizo makali, kukamatwa kwa viongozi na wanazuoni, pamoja na vitisho dhidi ya uwepo wao, haviwezi kamwe kuwalazimisha wananchi hawa kukubali maagizo wala kunyenyekea mbele ya udhalilishaji.

Kwa mujibu wa maelezo ya baraza hilo, uimara huu haumaanishi kupenda mauti, bali ni uamuzi wa kupata haki ya kuishi kwa heshima na kuwepo kikamilifu bila utawala wa kigeni wala utumwa wa ndani.

Muungano wa Mapinduzi wa Bahrain ulisema kwamba; “mtawala dikteta Hamad”, kwa mujibu wa maneno yake mwenyewe katika hotuba ya tarehe 30 Aprili 2026, anaongoza vita vya wazi nchini humo chini ya jina la “usafishaji”, jambo ambalo ni kukiri moja kwa moja nafasi yake katika aina zote za jinai zinazofanyika Bahrain, zikiwemo usafishaji wa kikabila, mauaji ya kitamaduni na mateso ya kidini.

Kwa mujibu wa muungano huo, amempa Waziri wa Mambo ya Ndani “Rashid Al Khalifa”, ambaye wamemtaja kuwa gaidi, ruhusa kamili ya kutekeleza mipango na maamuzi yanayohusiana na mauaji, mateso na uhamisho wa kulazimishwa, huku akitumia ushirikiano wa kiusalama kati ya tawala zinazofanya mapatano na zile wanazoziita za usaliti katika eneo hili.

Muungano wa Mapinduzi ulisisitiza kwamba; vita dhidi ya Mashia nchini Bahrain vinaendelea katika ngazi zote na kwa kutumia mbinu ambazo sheria za kimataifa huzitambua kuwa ni za kijinai, miongoni mwa mbinu hizo ni kunyang’anywa uraia, kufukuzwa kwa pamoja na kwa lazima, kuwakamata wanazuoni wakuu, kuinyima jamii viongozi wake, kuhalalisha uhalifu dhidi ya itikadi na nembo za kidini, udhibiti wa serikali juu ya mimbari na misikiti, kufungwa kwa taasisi za kidini, na juhudi za kufuta utambulisho wa kihistoria wa Mashia pamoja na kuharibu athari zao za kimada na kiroho, kwa matumaini ya kuwageuza kuwa kumbukumbu ya kihistoria isiyotambuliwa na inayotoweka polepole.

Katika sehemu nyingine ya taarifa hiyo imeelezwa kuwa; wananchi, wanazuoni na watu wema wa Bahrain hawatasimama bila kufanya chochote katika makabiliano haya ya hatima, kwa sababu hali ya sasa nchini Bahrain na eneo la Ghuba inaonesha kuwepo kwa mapambano halisi ambayo yataandika hatua inayofuata ya historia; hatua ambayo ndani yake hakutakuwa na nafasi kwa madola yenye kiburi, wakoloni na mawakala wasaliti, na ambapo mataifa huru yatatoa kauli yao ya mwisho kuhusu mwelekeo na mwisho wa makabiliano hayo.

Muungano huo ulisisitiza kwamba; medani ya makabiliano dhidi ya “Aal Khalifa” haitabakia kuwa na mipaka, kwa sababu moto wake hautabakia Bahrain, wananchi wake na Mashia wake pekee, hii ni kwa sababu “mtawala dikteta Hamad” amechagua kujipanga ndani ya mhimili wa Kizayuni na Marekani na ameonesha wazi uadui wake kamili dhidi ya mhimili wa muqawama na uongozi wake katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Lebanon, Yemen na Iraq.

Muungano wa Vijana wa Mapinduzi ya Februari 14 uliongeza mwishoni mwa taarifa yake kwamba; kikao cha “mtawala dikteta Hamad” na baraza lake dogo la mawaziri hakikuwa tu kwa ajili ya kusimamia vita dhidi ya Mashia wa Bahrain, bali pia kwa ajili ya kujadili hatari za kweli zitakazomzingira katika Kasri la Al-Safriyah.

Taarifa hiyo iliutaka “mkusanyiko huu wa kihalifu” kukumbuka, wakati wanaendelea kukiuka matukufu na misingi mitakatifu ya nchi, ule “usiku wa maamuzi ya mwisho” ambao utashuhudia kukimbia kwao kwa mwisho; siku ambayo si uhalalishaji wa mahusiano, si kambi za kijeshi, wala si falme zilizogeuzwa kuwa za Kizayuni zitakazowafaidisha kwa chochote.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha